Baadhi ya wageni mbalimbali na waandishi wa habari
wanaohuduria tamasha la ZIFF 2014 linaloendelea kutimua vumbi visiwani
Zanzibar.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).
Na. Mwandishi wetu.
BAADA ya kutoa demo katika mkutano wake na waandishi wa
habari, mkali wa rege nchini Innocent Nganyagwa ameahidi kuporomosha muziki
mzito katika ukumbi wa mambo klabu leo usiku.
Katika demo ambapo alipiga verse ya gila, mkali huyo
aliwataka wazanzibari kuingia kwa wingi kuona sweet reggae baada ya mfumo wa
Babylion wa ukombozi kumalizika.Anasema kwamba wapenzi wake watarajie vitu
vipya kuonesha kwamba yeye hajalala kwa miaka yote hata baada ya kuonekana kuwa
nje kwa miaka 9.Nganygwa mwenye tuzo tano za nyumbani na albamu nne katika
mikono amesema kwamba kimya chake kilitokana nba kuamua kusuka kizazi kipya cha
rege kupitia kampuni yake ya Reggae Production.
Akizungumza kuhusu muziki wake alisema kwamba yeye anapiga
muziki wa rege lakini si kwa mtazamo wa Jimmy Clief,Bob marley na Burning Spear
; ni muziki wenye utamaduni wa nyumbani na hivyo kwua na rege yenye utambulisho
wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment