MINI ZIFF 2013 inafanyika sambamba na Sherehe
za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Tamasha hili dogo litafanyika tarehe 10 -12
Jan, 2014 na kama kawaida ZIFF itatoa tuzo 10 za Filamu kwa waliofanya vizuri
kwa mwaka 2013 katika filamu za Kiswahili (Bongo Movie). Tuzo zitakazotolewa ni
Muigizaji Bora wa Kiume na Kike, Muongozaji Bora, Filamu Bora ya Mwaka,
Muigizaji anayechipukia, Filamu bora katika Sauti, Filamu bora katika Hadithi,
Balozi bora wa Filamu za kitanzania, Kampuni au mtu aliyetoa mchango mkubwa
katika Tasnia hii kwa mwaka huu na Tuzo ya Heshima. Tamasha hili dogo litajumuisha
filamu za kitanzania peke yake (Bongo
movies) ilikuendelea kutoa mwamko kwa watengenezaji filamu wa Tanzania kufanya vyema
katika tasnia hii, Tamasha hili ni utangulizi wa tamasha kubwa la ZIFF
litakalofanyika 14 – 22 Juni, 2014.
Mini ZIFF
itaonesha filamu kwa siku mbili na siku ya mwisho Tuzo zitatolewa kwa
walioshinda, pia tunategemea kuwaalika wasanii mbalimbali maarufu kutoka hapa
Tanzania kama JB, Cloud, Steve Nyerere, Ray, Makombora, Simon Mwakifamba,
Monalisa, Wema Sepetu, Irene Uwoya, Lulu na wengine wengi.
Pia tunategemea kufanya show kabambe ya
muziki baada ya kutolewa kwa tuzo, wasanii watakaopanda jukwaani watatangazwa
hapo baadae. Kwa wale wote wanaotaka kuleta kazi zao basi walete sasa ila ziwe
ambazo zimetoka mwaka 2013 tu. Wasiliana na Ibra 0713300997(DAR) au Mohd
0778685676 (ZNZ).
MINI ZIFF 2013 inaletwa kwa udhamini mkubwa
wa ZUKU, Push Mobile, Azam Marine, Filamu Central Clouds TV kupitia kipindi cha
Take One na Clouds FM kupitia kipindi cha Leo Tena.
No comments:
Post a Comment