Pages

Saturday, June 21, 2014

ADY BATISTA WA “THE THORN OF THE ROSE” AKONGA NYOYO ZA WAPENZI WA SINEMA TAMASHA LA ZIFF 2014

DSC_0128
ADY de Batista (30).
DSC_0154
ADY de Batista akisaidiwa kushuka kwenye gari na meneja wake Sholey Maqueta mara baada ya kuwasili kwenye viunga vya Ngome Kongwe visiwani Zanzibar. (Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
ADY de Batista alishuka taratibu katika gari la Noah, akiwa amevalia nguo nyeupe.Alisaidiwa kushuka kwenye gari na meneja wake Sholey Maqueta na kuingia katika ukumbi wa maonesho ya sinema wa wazi uliopo Ngome Kongwe kwa ajili ya sinema yake ya O Espinho Da Rosa.
Kutoka kwenye gari hadi alipopokewa na Mtendaji wa tamasha la Filamu la Kimataifa la Zanzibar (ZIFF) Profesa Martin Mhando,unamuona mdada anayejiamini, mwenye uzuri wa asili na weusi unaong'aa majira ya magharibi kabisa, kabla ya swala ya insha.
DSC_0157
ADY de Batista akiingia kwenye lango kuu la Ngome Kongwe.
Alikuwa anatembea taratibu kama malkia kushoto akiwawepo meneja Sholey na Kulia rafiki yake wa kiume Antoine Simonet.Nyuma alikuwapo mdogo wake Nautenle Batista.
Alipokewa na Mtendaji wa ZIFF Profesa Martin Mhando ambaye alizungumza kidogo kuhusu O Espinho Da Rosa (The Thorn Of The Rose) kabla ya kumkaribisha kuzungumza na wapenzi wa sinema waliokuwa wamejazana pomoni katika ukumbi wa sinema.
DSC_0181
ADY de Batista na Meneja wake wakielekea kwenye jukwaa la ZIFF 2014 kuhutubia.
Kabla ya kuzungumza kuhusu filamu hiyo ambayo imechezwa na JĂşlio Mesquita, mwenyewe Ady Batista, Daniel Martinho, Ă‚ngelo Torres na Ciomara Morais, Ady alishukuru kuwepo Zanzibar na kusema kwamba ndoto yake imetimia, anashukuru sana.
Sinema hii ambayo ni saa moja na dakika 37, ni sinema yenye makali yote ya maisha, mashaka na pia imani zilizojikita vyema katika jamii ambayo imekuwa ikikabiliwa na matatizo mbalimbali.
DSC_0194
ADY de Batista akizungumzia filamu yake.
Maneno ya ndoto kutimia yameonesha furaha aliyoiandika katika mtandao wa kijamii wa Facebook Mei mwaka huu baada ya kuambiwa kwamba filamu yake imeingia katika mashindano ZIFF.
Katika hiyo face book ya Mei mwaka huu aliandika: E nĂłs fomos seleccionados! JĂşlio Mesquita Audilia Batista Daniel Martinho Daniel Martinho Angelo Torres Ciomara Morais Sonia Claudia Neves Eric Santos Eric Santos akimaananisha : Tumechaguliwa! akiwataarifu JĂşlio Mesquita Audilia Batista Daniel Martin Daniel Martin Angelo Torres Noelle Matthews Sonia Santos Santos Eric Eric Claudia Neves .
DSC_0186
Shangilio lililokuwa katika facebook ndilo hasa alilolionesha wakati akizungumzia sinema yake hiyo ambayo ilipigwa picha kwa siku 20 na kutoa matokeo kama sinema ya Hollywood kwa ubora.
Ikiwa inajulikana kama The Thorn of the Rose,kwa kingereza, filamu hii ambayo ilikuwa ya kwanza kwa mtengeneza sinema Filipe Henriques ipo katika maelezo ya ushindani ambayo yanatoa ubora wa picha na skripti yenyewe kwa namna ambavyo matukio yamefungwa pamoja na kuwa kama visa zaidi ya viwili katika filamu.
DSC_0207
Kiukweli wakati natazama sinema hii Ngome Kongwe na hata katika maonesho binafsi ya ndani ya ukumbi wa kujitegemea Double Tree Hotel, ina wakati inakuchanganya mwenendo ambao unatakiwa kuwa nao makini kwani kuna muda unajisikia kama kutapika kwa hasira wakati mtengeneza sinema alipokuwa akiiperemba jamii na makovu ya wanasiasa.
Unaweza kusema kwamba simulizi hili lina mashetani, lakini masimulzii yake yanakupa neno jema kabisa la kuzungumza wakati ukimaliza kuona sinema hii.
Mwendesha mashtaka David Lungha (JĂşlio Mesquita) katika filamu hii anakutana na binti mrembo ambaye uwepo na utokeaji wake ni wa 'utata' zaidi anayekwenda kwa jina la Rosa (Ady Batista).
Hawa wawili wanakutana katika baa ambapo watu walikuwa wanamsubiri kumpa hongera kwa ushindi wake mahakamani. Amabo anaukiri na kusema mapambano yanaendelea.
Akisema hivyo anakwenda kukaa katika kiti cha baa na pembeni mwake kuna askari polisi.
Akiketi pale mmoja wa wasaidizi wake anafika kwake akionekana wazi si tu kutoa hongera bali kumtaka kimapenzi na kumkataa, lakini akiondoka analetewa bahasha na mtandia , lakini kabla ya hapo anazungumza na polisi ambaye anamwambia hakuna ua waridi lisilokuwa na miba na ogopa unapopata ua waridi tatu.
Akaondoka akmfyonza lakini kweli aliona kuna ua waridi na maneno ya polisi yanaweza kuwa kweli.
DSC_0230
Muda mfupi tunasikia kishindo cha kiatu na anaingia binti wa kike ambaye mwendesha mashtaka anaingiwa na kwikwi na wanaanza mambo ambayo yanapeleka katika mtandao mkubwa zaidi wa uwongo, kusalitiana, mauaji na rushwa.
Ukiangalia sinema hii hata mwanzo unapata maswali mengi kama kweli Rosa ni mtu kweli au ni mawazo ya mwendesha mashtaka, ama ni mzimu ambao hauwezi kutulia kuzimu mpaka habari ya kifo chake ielezwe.
katika simulizi hili muigizaji kinara David Lungha ni mwanamume mwenye mvuto mkubwa wa kimapenzi lakini mtata; na mtu wetu wa leo katika sebule la sinema Ady Batista ni mdada mzuri, ambaye anaonekana kuchukua kiatu cha Rosa, kama asiyekuwa na raha huko aliko.
Ndani humu Eric Santos ni askari ambaye amekuwa polisi akiwa na siri nyingi mbaya za kwake.
Lakini msimuliaji wetu anataka kukueleza kwamba si sahihi kuacha kurekebisha mambo na wale waliokufa, kwani hutafuta njia ya kurudi na kurekebisha mambo yao, imani ambayo Waguinea wanayo sana.
Mapenzi ya mwendesha mashtaka David Lunga kwa Rosa kuna vuruga kila kitu na Lunga anajikuta akifanya vitu vingi kwanza kumaananisha kwamba hana kosa wala hana sababu ya kujuta.
DSC_0248
Filamu hii ambayo iliwapa shida watu wa sensa wa ZIFF ili iweze kuonwa na watu wengi ukumbi wa wazi, unazungumzia kwa namna ya pekee rushwa, ubakaji ambao unafanywa katika maisha ya binti, kifo chake na jinsi ambavyo anataka jumuiya ijue.
Pamoja na kwamba binti alikufa katika utata wa kutoa mimba alirejea duniani kutafuta msaada wa haki kutendeka na katika hili Polisi yule (askari wa zamani) aliwaua lakini akashindwa kummaliza moja kwa moja Lunga ambaye alimuua.
Kiukweli kuelekea mwisho wa sinema unaona matukio mengi na jinsi hali ilivyo ngumu na lazima aifanyie kazi.
Filipe Henriques ameifanyakazi kubwa sinema hii ambayo imejaa usaliti kuanzia wa kisiasa, kijamii hadi kimapenzi huku mazungumzo yakiwa mapenzi kwa watoto wadogo.
Lugha ya kireno ambayo imeambatana na lugha ya kiingereza katika maandishi yanayopita si nzuri kihivyo, lugha ina matusi mengi na isiyopendeza na kuna grafiki za mapenzi ya kulazimishwa katika hali isiyokubalika.
DSC_0249
ADY de Batista akiondoka mara baada ya kumalizika kwa filamu yake.
Mdada huyu ambaye katika mazungumzo alisema kwamba simulizi la sinema ile ni matukio ya kweli nyumbani kwao ambapo pia kuna imani kubwa kuhusu mizimu kurejea duniani pamoja na kuwapo dini ya Kikristo na Kiislamu,ametaka jamii kujipambanua na maradhi ya woga na kuchukua hatua kwanza binafsi na kisha kijamii dhidi ya maovu.
Mdada huyu ambaye hajaolewa lakini ana rafiki wa kiume, alikuwa Zanzibar na mdogo wake na Meneja wake.
Mdogo wake ndiye anayejua kiingereza kwa ufasaha zaidi huku yeye mwenyewe amebahatisha.
Nilipomuuliza kuhusu nguo yake nyeupe, kwani katika sinema kuna vazi la harusi, alisema rangi nyeupe ni alama ya matumaini.
DSC_0257
Kuendelea kusoma zaidi bofya hapa

Thursday, June 19, 2014

MZUNGU KICHAA NA RICO SINGLE KUKINUKISHA LEO ZANZIBAR LIVE!!

 Music Coordinator wa ZIFF, Edward Lusala akiwatambulisha wasanii watakaotumbuiza usiku wa leo kwenye tamasha la 17 la ZIFF 2014 ndani ya viunga vya Mambo Club - Ngome Kongwe visiwani Zanzibar wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Katikati ni msanii wa muziki nchini almaarufu kama Mzungu Kichaa na Kulia ni Msanii Grace Matata.
 Mzungu Kichaa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Doubletree by Hilton, ambapo amelishukuru tamasha la ZIFF 2014 kwa kutoa nafasi kwa wasanii wanaoimba Live Music kuonyesha uwezo wao kwenye tamasha hilo linaloukutanisha watu mbalimbali kutoka kila kona ya dunia ikiwemo na kubadilishana uwezo na wasanii wengine wa nje.
 Msanii wa muziki wa Bongo flava visiwani Zanzibar almaarufu kama Rico Single, akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameahidi kuwapa raha ya Live Music kupitia bendi ya BODY, MIND & SOUL  kutoka nchini Malawi itakayokuwa ikimpigia vyombo, vilevile amewapongeza waandaji wa tamasha hilo kwa kuwapa nafasi na kuwatangaza wazawa kimataifa kupitia tamasha hilo
 Baadhi ya wasanii wa filamu na muziki wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Doubletree by Hilton visiwani Zanzibar.

Wednesday, June 18, 2014

INNOCENT NGANYAGWA KUTUMBUIZA TAMASHA LA ZIFF 2014 USIKU HUU NDANI YA UKUMBI WA MAMBO CLUB, NGOME KONGWE

 Mwanamuziki Mkongwe wa Rege nchini, Innocent Nganyagwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na show yake kwenye tamasha la ZIFF 2014 usiku wa leo ndani ya ukumbi wa Mambo Club kwenye viunga vya Ngome Kongwe visiwani Zanzibar.Kushoto Mtaalamu wa masuala ya habari ZIFF, Bw. Dave Ojay.
Baadhi ya wageni mbalimbali na waandishi wa habari wanaohuduria tamasha la ZIFF 2014 linaloendelea kutimua vumbi visiwani Zanzibar.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).

Friday, June 13, 2014

ZANZIBAR INTERNATIONAL FILM FESTIVAL>> ZIFF>> - A FEAST OF FILM, MUSIC & VISUAL ART



The Zanzibar International Film Festival 2014 is host to more than film screenings. The 8 day line-up also includes nightly musical performances, visual art exhibitions and more. The focus on Swahili arts & culture is an important element of the festival, especially in light of the historical lack of Swahili art exhibitions.

The music programme is a celebration of the African sound, with top artists from across the continent including Didier Awadi from Senegal, Habib Koite from Mali, and Tanzania’s AY.

Opening Weekend & Women’s Panorama

Opening Parade
June 14th 15:00 Benbela School – Old Fort
Join in the festivities as we officially kick-off ZIFF 2014. The theme for this year’s parade is A Common Destiny – Unite Against Gender Based Violence.

Dhow Race
June 15th, Tembo Hotel Beach 14:00
One of ZIFF’s most popular attractions, come cheer on the Dhows as they race in this exciting event.
 Market & Chill Out CafĂ© – Daily from 10am – 4pm
House of Wonders
Explore the wares on-sale from the women vendors of Zanzibar. Daily entertainment includes the following:

June 17th: Kidumbak Performance
June 18th:  Mrembo tips and tricks 14:00
June 19th: Fashion Show 15:00
June 20th: Music Performance
June 21st: Kidumbak Performance 
June 22nd: Puppet Show

Visual Arts

“Swahili Gift” an Exhibition by Seif Soud
Monday June 16th – 22nd June Double Tree Hilton Hotel
Seif Soud is a Zanzabari born and bred artist who began performaning his craft in 1999 in the Ngome KOngwe Art Precinct in Stonetown Zanzibar.

In this exhibition he paints sites and images that are inspired by Swahili cultural materials, colours and way of life, which fuses to create a lasting impact on the viewer.

Afrika Tutafika Exhibition
June 15 – 18th Old Customs House
This exhibition from the Ugandan design house features African inspired fashion that are made in Uganda from locally sourced materials.



Sisygambis
June 19th – 22nd Old Customs House
With this creation on 3 screens, Christine Coulange achieves a long-term multimedia work : 5 years of travel, sound recording, sound and images composition while following musicians, rites and ceremonies in the deserts and the villages, in the islands and the cities all along this big geographic arc which joins up the Mediterranean sea and the Indian Ocean.

It is long journey across the Spice Road, a wide crossing full of sonorous images, rhythms from Egypt to Laos and Malaysia, through Tanzania, Kenya, the Comoros and Zanzibar. We follow the vital lead of rituals, rare and powerful, overwhelming landscapes, every day’s life details… Eyes and ears open to actions and rhythms, to collective ritual practice, to body language, to echoing threnodies, Sisygambis sew together traditional music and surrounding sounds to their own electronic compositions.

Transported by trance music and seams from ancestral and contemporary cultures, the film makers-composers want to transmit through musical and visual sampling the power of gestures, the singularity of ordinary and extraordinary voices, the strength and the beauty of men and women at the other end of our common world.

Music & Performance

Music-wise the festival will feature 13 performing groups with Didier Awadi, the Senegalese maestro performing on the opening night on 14th June. Live music followed by DJ’s will take place every night after the main movie screening in the Old Fort.

Groups from Tanzania, Kenya, Uganda, Malawi and Egypt are scheduled to entice audiences over the 9 nights of the festival.

All concerts will take place at the Old Fort and tickets are available online at www.ziff.or.tz

June 14th. Tamaduni Music (Tanzania), Didier Awadi (Senegal)
June 15th: Cocodo Band (Tanzania), Sauti Sol (Kenya)
June 16th: Raha-T- Zamani (Zanzibar), Warriors From the East (Kenya/Tanzania), Tanuri Group (Egypt)
June 17th: Sisi Na Wew, Madame Faki / Kidumbak (Zanzibar)
June 18th: DCMA (Zanzibar), Ras Innocent Nganyagwa Tanzania)
June 19th: Rico Single (Zanzibar), Mzungu Kichaa (Zanzibar/ Tanzania)
June 20th: Smile (Zanzibar),Grace Matata (Tanzania),  Comoros, Makamando
June 21st : ZIFF After Party with Godykaozya & The Tongwa Ensemble (Tanzania), Habib Koite (Mali)
June 22nd: AFDA After Party with AY(Tanzania), Body, Mind & Soul (Malawi), AY (Tanzania)

Online Ticket Purchases
All evening concert event tickets can be purchased in advance conveniently via 3G Directpay, which will provide with the online payment service for the nine-day bounty of special programming and festivities. Passes will be available for purchase at www.ziff.or.tz .

About ZIFF

The Zanzibar International Film Festival is the longest running film-festival in East Africa, with global credibility and instant Pan-African recognition.
The ZIFF Festival of the Dhow Countries is organized by ZIFF, a non-governmental, non-profit organization founded in 1998 in Zanzibar to promote and showcase the culture of the Dhow Countries. Every cent raised from sponsors and donors ensures the widest possible accessibility of high- quality international screenings and cultural events to all sections of the Tanzanian population.
The ZIFF Festival of the Dhow Countries is a catalyst for the promotion and development of the region’s cultural industries. It encourages and supports the development of artistic skills and the infrastructure necessary for a vibrant and innovative arts environment.
The festival programme gives particular prominence to the visibility and interests of women and children, including the youth.
The main panorama features international film and video screenings, and international retrospectives along with music and performances, main stage events, exhibitions, workshops and seminars.
Emphasis has been given to The East African Film Makers forum and this will continue in Festival 2014, as will dialogues with various filmmakers from across the region.


For more information: www.ziff.or.tz, www.facebook.com/zanzibarinternationalfilmfestival, @ZIFF_2014 #ZIFF2014