Pages

Friday, February 14, 2014

Sauti za Busara 2014 zazidi kuinogesha zanzibar.

 

Na Andrew Chale, Zanzibar.
 
MWANAMUZIKI nguli wa miondoko ya Afro rege, Jhikoman Manyika   jana usiku Februari 13,  aliwasha moto  kwa kupiga shoo ya nguvu iliyodumu kwa lisaa limoja na kukonga nyoyo umati mkubwa uliojitokeza kwenye tamasha hilo la 11,la Sauti za Busara mwaka huu 2014. Jhikoman alipanda jukwaani majira ya saa tatu usiku  sambamba na bendi yake ya Afikabisa na kupiga vionjo mbalimbali vya nyimbo zake za sasa na za nyuma.

Jhikoman aliweza kuwasha moto huo kwa kupiga nyimbo zake zilizopo kwenye albamu yake ya Chikonda na nyingine hali iliyokonga wadau hao wa muziki wakiwemo wageni kutoka mataifa mbalimbali na watanzania waliojumukika kwenye tamasha hilo.

Hata hivyo, Jhikoman alisema baada ya shoo hiyo anatarajia kupiga shoo zingine kwenye nchi mbalimbali kwa kufanya ziara maalum ikiwemo mataifa ya Ulaya. Mbali na Jhikoman wasanii wengine ni pmoja na kundi la Seven Survivor wanopiga muziki wa mchiriku, huku kundi la Baladna taarabu wao walikonga nyoyo kwa muziki wa mwambao na taarabu asili. Wengine ni kundi la Pongwa kutoka visiwani Zanzibar,  Tritonik (Motius), na nyingine nyingi.

Awali tamasha hilo lilifunguliwa kwa paredi iliyokusanya wanamuziki mbalimbali kutoka mataifa yote na kwa kila mmoja kuonyesha muziki wake mitaani na kasha kumalizikia kwenye viunga vya Ngome Kongwe. Aidha tamasha hilo la siku nne, linatarajiwa kuwa na wanamuziki mbalimbali vikiwemo vikundi 32, vyenye jumla ya wasanii 200, ambao watapiga shoo kwenye jukwaa hilo la Kimataifa. Hadi sasa mji wa Zanzibr umebarikiwa kuwa na wageni mbalimbali wakiwemo waliofika maalum kwa ajili ya shoo na wale wanaokuja kupumzika kwenye kisiwa hiki cha marashi ya karafuu.Aidha, tayari idadi ya wageni imeongezeka  huku baadhi ya hoteli zikiwa zimefurika  na biashara za kitalii zikiwa zinanunuliwa kwa wingi.

Kwa upande wake, David Ojoy ambaye ni msaidizi wa masuala ya habari wa tamasha hilo, anasema kuwa  hali ya wageni imekuwa kubwa kufika kwenye tamasha hilo ikiwemo kupata habari mbali mbali zinazoptikana kwenye mtandao maalum wa tamasha hilo pamoja vyombo vya habari. "Tunavipongeza vyombo  vya habari kwa kutupa sapoti na tunaomba tuendelee hivyo hivyo ilikukuza muziki wetu wa kiafrika na kujenga tamaduni imara hapa afrika na tamasha hili liendelee kuwa la kimataifa zaidi" alisema Ojay.

Friday, February 7, 2014

SAUTI ZA BUSARA 2014: THE LINE UP



anDizu Plaatjies & The Ibuyambo Ensemble
Street Rat and Body Mind & Soul
Seven Survivor

 Tamasha la Sauti za BUSARA ZANZIBA LINATARAJIWA KUFANYIKA 13 -16 February hii 2014. List ya watakaotoa burudani ni kama ilivyo

Jupiter & Okwess International (DRC)  Ebo Taylor (Ghana / Germany)  Joe Driscoll and Sekou Kouyate (USA / Guinea)  Waldemar Bastos (Angola / Portugal)  Sona Jobarteh (Gambia / UK)  The Nile Project (Nile Basin)  Noumoucounda Cissoko (Senegal)  Wunmi (Nigeria / UK / USA)  Dizu Plaatjies & The Ibuyambo Ensemble (South Africa)  Addis Acoustic Project ft Melaku Belay (Ethiopia)  OY (Ghana / Switzerland)  Tausi Women's Taarab (Zanzibar)  Seven Survivor (Tanzania)  Street Rat and Body Mind & Soul (Malawi)  Tarabband (Egypt / Sweden / Iraq)  Baladna Taarab (Zanzibar)  Majestad Negra (Puerto Rico)  HAJAmadagascar and The Groovy People ft. Werner Puntigam (Madagascar / France / Austria)  Jhikoman (Tanzania)  Hoko Roro (Tanzania)  Ashimba (Tanzania / Finland)  Swahili Vibes (Zanzibar)  Tritonik (Mauritius)  Kara Sylla Ka (Senegal / Switzerland)  Joel Sebunjo (Uganda)  Abantu Mandingo (Tanzania)  Segere Original (Tanzania)  Moyize (Rwanda)  Ricky na Marafiki (Kenya)  Rajab Suleiman & Kithara ft. Derya Takkali (Zanzibar / Turkey / Germany)  Kazimoto (Tanzania / Germany)  Swahili Encounters Group (Zanzibar / Tanzania / Various)  Pungwa (Zanzibar / Tanzania)  and more

Thursday, November 21, 2013

(News) Mini ZIFF na Filamu za Bongo

MINI ZIFF 2013 inafanyika sambamba na Sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Tamasha hili dogo litafanyika tarehe 10 -12 Jan, 2014 na kama kawaida ZIFF itatoa tuzo 10 za Filamu kwa waliofanya vizuri kwa mwaka 2013 katika filamu za Kiswahili (Bongo Movie). Tuzo zitakazotolewa ni Muigizaji Bora wa Kiume na Kike, Muongozaji Bora, Filamu Bora ya Mwaka, Muigizaji anayechipukia, Filamu bora katika Sauti, Filamu bora katika Hadithi, Balozi bora wa Filamu za kitanzania, Kampuni au mtu aliyetoa mchango mkubwa katika Tasnia hii kwa mwaka huu na Tuzo ya Heshima. Tamasha hili dogo litajumuisha filamu za kitanzania peke yake  (Bongo movies) ilikuendelea kutoa mwamko kwa watengenezaji filamu wa Tanzania kufanya vyema katika tasnia hii, Tamasha hili ni utangulizi wa tamasha kubwa la ZIFF litakalofanyika 14 – 22 Juni, 2014.
  Tuzo zitatolewa baada ya jopo la majaji kupitia kazi zilizoletwa kwaajili ya Mini ZIFF na pia Tuzo ya Muigizaji Bora wa Kiume na Kike zitapata kupigiwa kura na wananchi kupitia namba maalum itakayotolewa hapo baadae kupitia Puch Mobile na hivyo kufanya watu wote Tanzania nzima kupiga kura.
 
Mini ZIFF itaonesha filamu kwa siku mbili na siku ya mwisho Tuzo zitatolewa kwa walioshinda, pia tunategemea kuwaalika wasanii mbalimbali maarufu kutoka hapa Tanzania kama JB, Cloud, Steve Nyerere, Ray, Makombora, Simon Mwakifamba, Monalisa, Wema Sepetu, Irene Uwoya, Lulu na wengine wengi.
Pia tunategemea kufanya show kabambe ya muziki baada ya kutolewa kwa tuzo, wasanii watakaopanda jukwaani watatangazwa hapo baadae. Kwa wale wote wanaotaka kuleta kazi zao basi walete sasa ila ziwe ambazo zimetoka mwaka 2013 tu. Wasiliana na Ibra 0713300997(DAR) au Mohd 0778685676 (ZNZ).
MINI ZIFF 2013 inaletwa kwa udhamini mkubwa wa ZUKU, Push Mobile, Azam Marine, Filamu Central Clouds TV kupitia kipindi cha Take One na Clouds FM kupitia kipindi cha Leo Tena.